Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948

Thursday 27 July 2023

Mkutani wa kimataifa wa Julius nyerere Dar es salaam

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, Rais wa Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera, Rais wa Madagascar, Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa São Tomé na Principe, Mhe. Carlos Vila Nova pamoja na Rais wa Sierra Leone, Mhe. Julius Maada Bio wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam Julai 26, 2023

Monday 24 July 2023

Matumizi ya Mtandao wa Threads yadaiwa kushuka kwa 75%

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Sensor Tower inayohusika na masuala ya utafiti wa Masoko ya Kimtandao, umebaini kuwa matumizi ya #Threads yameshuka kwa 75% ikiwa ni wiki chache tangu Mtandao huo kuingia sokoni. Threads ambayo ilifanikiwa kuweka rekodi ya kupakuliwa na watumiaji zaidi Milioni 100 ndani ya siku 5, na hadi sasa imepita watumiaji Milioni 184 imedaiwa kutokuwa na utofauti mkubwa na mshindani wake ambaye ni #Twitter. Imeripotiwa kuwa watumiaji wengi walioachana na Twitter tangu kampuni hiyo inunuliwe na Bilionea Elon Musk, wamejiunga na Threads, hata hivyo Threads haipatikani katika Nchi za Umoja wa Ulaya kutokana na Sheria kali za Ulinzi wa Taarifa Binafsi. =========== After a wildly successful first few days, Threads popularity has waned in the weeks since Meta launched its challenge to Twitter, which lives on despite its problems. The average amount of time people spend on Threads daily has plummeted more than 75 percent since the platform made a rock star debut on July 6, according to data from Sensor Tower, a market analysis firm. Threads was quickly billed as a potential death knell for Twitter, a platform that has tumbled into chaos under the leadership of mercurial tycoon Elon Musk. The launch saw sign-ups of more than 100 million users in less than five days, smashing the record of AI tool ChatGPT for fastest-growing consumer app and creating relief and excitement amongst early adopters fleeing Twitter. "I actually closed down my Twitter account after starting Threads," said Brooklyn resident Lauren Brose, head of marketing at a tech start-up. "I used to love Twitter. After Elon Musk took over Twitter, I found that the entire environment just changed completely." But weeks later, Threads has since seen a "material decline in new sign-ups," Sensor Tower said. Twitter continues to dominate its space as a platform for online comment and news, and Musk "would have to completely destroy it" to drive away its audience for good, according to Silicon Valley investor and analyst Jeremiah Owyang. "Will Threads kill Twitter? Absolutely not. It's just not equivalent," he said. Threads went live on Apple and Android app stores in 100 countries at its launch, though it is not available in Europe because parent company Meta is unsure how to navigate the European Union's data privacy legislation. Twitter is thought to have around 200 million regular users but it has suffered repeated technical failures since Tesla tycoon Musk bought the platform last year and sacked much of its staff. Musk, also the boss of SpaceX, has alienated users by introducing charges for previously free services and allowing banned right-wing accounts back on the platform. There is little doubt that Threads had a major leg up compared to other wannabe Twitter alternatives. Several rivals have emerged but most are niche platforms without the capacity to grow at the necessary scale to dethrone Twitter. But Meta was able to easily prompt Instagram users to start Threads accounts, tapping into a base of at least a billion users at the image-focused social network. Not about news? Threads has a lot to prove, and features to add, to become a formidable Twitter alternative, according to Insider Intelligence analyst Jasmine Enberg. It needs to foster creators to engage users, and to find its own identity separate from Instagram and Twitter, Enberg said. "Given that Twitter is in a state of disarray, the brilliant move that they did was using the existing social graph from Instagram for rapid and seamless adoption," Owyang said of Threads. The downside is that's not the user base "that you want to have chats with or to do microblogging," he added. Instagram users typically engage with the service for images or videos, not commentary or controversy, Owyang noted. "It is a very different crowd on Instagram," Creative Strategies analyst Carolina Milanesi said of a comparison to Threads. Twitter is known as a forum for news and politics, topics that Threads has no interest in spotlighting, according to a recent post by Threads and Instagram boss Adam Mosseri. Meanwhile, Twitter is seen as an established home for posts by journalists, celebrities, athletes, politicians and others.

Wednesday 19 July 2023

TMA yatahadharisha uwepo wa El Nino kwa Asilimia 90, Oktoba 2023

TMA imesema hadi sasa imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hasa kipindi cha mvua za msimu wa vuli zinazotarajiwa kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu katika maeneo mbalimbali nchini. Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) imesema El Nino inatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu ambazo zitasababisha athari katika maeneo mbalimbali nchini. Akitoa taarifa hiyo leo Jumatano Julai 19, 2023 Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema hadi kufikia sasa inaonyesha imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Dk Kantamla aliyataja maeneo ambayo yataathirika na mvua za El nino ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara "Ongezeko la mvua linasababisha kutabiri uwepo wa El Nino, mfano kipindi cha kipupwe tumeona imeanza kujitengeneza athari zake hatutegemei kipindi hiki ongezeko la mvua kubwa,"amesema Dk Kantamla. Pia, Dk Kantamla amesema El Nino haitaathiri wakazi bahari ya hindi pekee itasambaa hadi maeneo ya nyanda za juu Kaskazini na ukanda wa Pwani. “Katika kipindi hiki cha kipupwe TMA inaendelea kufuatilia kwenye mchakato wa kuelekea msimu wa mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba mwaka huu na kuangaliwa athari za El Nino kwa ufasaha Ili kuifahamisha jamii kwa ujumla,”amesema. Nini maana ya El Nino Ni hali ya uwepo wa ongezeko la joto la bahari ya katika eneo la kati ya kitropiki la bahari ya Pasifiki, hali hii inapokuwepo kunakuwa na madhara mbalimbali katika maeneo tofauti ya duniani.

Sunday 16 July 2023

Ripoti ya Uwajibikaji wa Vyombo vya Usimamizi kwa Taasisi za Umma 2021|22

Hali ya Utekelezaji wa Mapendekezo ya CAG kwa Miaka 3 hairidhishi 1689077120507.png Ripoti ya Uwajibikaji ya Taasisi ya Wajibu Institute imebainisha kuwa kwa kipindi cha Miaka Mitatu, (2018/19-2020/21), utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kikamilifu bado upo chini ya asilimia 50 Swali la msingi ni, kwa nini hakuna msukumo wa kutekeleza mapendekezo ya CAG? 1689142986449.png Mapendekezo yanayotolewa na CAG yanalenga kuboresha mifumo ya usimamizi/ uwajibikaji na utendaji wa Serikali. Kutotekelezwa kwa mapendekezo ya CAG kwa wakati, kunafanya madhaifu yaliyobainishwa kuendelea kuwepo na wakati mwingine kuisababishia Serikali hasara. 1689230057140.png Matokeo ya ukaguzi wa CAG kwa kipindi cha Miaka mitatu (2019/20 – 2021/22) yanaonesha maboresho katika uandaaji wa hesabu kwa Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa Hii imepelekea kuongezeka kwa idadi ya Taasisi, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaliyopata hati safi kutoka 87% mwaka 2019/20 hadi kufikia 96% mwaka 2021/22 Hata hivyo bado kuna mapungufu kama, kutozingatiwa matakwa ya Sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi yaliyopelekea uwepo wa viashiria vya upotevu wa fedha na rasilimali za umma Mapendekezo: WAJIBU inaendelea kushauri yafuatayo; a. Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ipendekeze kufanyika kwa marekebisho kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 ili kuweka kifungu kitakacho weka adhabu zikiwemo hatua za kinidhamu kwa Maafisa Masuuli ambao hawajatekeleza mapendekezo yanayotolewa na CAG katika kaguzi za fedha ambayo hayahitaji mabadiliko ya kisheria au mapendekezo yaliyo ndani ya uwezo wa maafisa masuuli. Hii itawaongezea wakaguliwa msukumo, hamasa na ari ya kutekeleza mapendekezo ya CAG. b. Serikali kupitia Taasisi ya Serikali Mtandao (eGA) iunganishe mfumo wa GARI- ITS na IFT - MIS ambayo inatumika sasa kufuatilia utekelezaji wa mapendekezoya CAG katika mashirika ya umma na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Mifumo hii miwili iunganishwe ili kuwe na mfumo mmoja ulio wazi na madhubuti utakaotumika kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG. c. WAJIBU inashauri, Ofisi ya CAG itoe mapendekezo yake kwa mchanganuo wa mapendekezo ya muda mfupi, kati na mrefu ili kurahisisha utekelezaji na ufuatiliaji. d. WAJIBU inashauri CAG kutoa mchanganuo wa mapendekezo yaliyo ndani ya uwezo wa maafisa masuuli na yale yanayohitaji mabadiliko mapana ya kisera, kisheria na miongozo mbalimbali. Mchanganuo huu ubainishe muhusika mkuu katika kutekeleza mapendekezo maususi na namna ya kumuwajibisha. Attachments

16/7 jumapili hii dau la habari

 https://youtu.be/btvQtsH5X6Y

AWE yawapatia mafunzo wanawake kuwa Wajasriamali bora Afrika Mashariki

 Naye balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wajasriamali wanawake kukutana na kupeana elimu juu ya masuala ya kijasiriamali ili kumaliza umasikini katika ukanda huo ya wa Afrika mashariki.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle.

Balozi huyo wa Marekani alisema,“ni muhimu kwa wanawake wajasiriamali kupata nafasi ya kuungana kwa pamoja na njia pekee ya kumaliza umaskini katika Afrika Mashariki ni kuwa na wanawake wenye nguvu sana ambao wanajihusisha na biashara zinazoungwa mkono na taifa lao na kuungwa mkono na wanaume wa taifa lao pia hii inaleta tofauti katika kupanda kwa mtu binafsi na inafanya tofauti katika kukua kwa taifa.”

Hata hivyo mkufunzi na mjasiriamali Victoria kisyombe, alimalizia kwa kusisitiza nchi za Afrika kutambua umuhimu wa mwanamke kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi kwani kumuendeleza mwanamke ni kuendeleza familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Imetayaraishwa na Amri Ramadhani Sauti ya Amerika, Dar es salaam.

Saturday 15 July 2023

MARUFUKU KUFAA MAVAZI YANAYOFANANA NA YA KIJESHI


 Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limesema Katika siku za karibuni kumeibuka makundi ya watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya walinzi wa viongozi wakivaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama.


Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, kinakataza mtu yeyote ambaye si askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za majeshi ambapo ameongeza kuwa sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza pia.

Amesema Jeshi la Polisi Tanzania linawataka wale wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kinyume na sheria za nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitasita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Misime ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelee kuiweka nchi salama.

#2skys_updates 

Thursday 13 July 2023

Kwanini Bollywood bado inatengeneza filamu zenye 'kudhalilisha wanawake na mawazo ya kizamani'

 Kwanini Bollywood bado inatengeneza filamu zenye 'kudhalilisha wanawake na mawazo ya kizamani'

July 13, 2023
Bollywood, tasnia maarufu ya filamu ya Kihindi nchini India, mara nyingi hufafanuliwa kama ulimwengu wa mwanamume.
Ni jambo ambalo limekuwa likizungumzwa kwa muda mrefu, lakini sasa utafiti mpya unaonyesha jinsi usawa wa kijinsia ulivyo – kwenye skirini na nyuma ya pazia.
Sekta ya $2.1bn (£1.5bn) huzalisha mamia ya filamu kila mwaka na ina wafuasi wengi miongoni mwa Wahindi duniani kote.
Nguvu ya filamu na waigizaji nyota kwenye mawazo ya mashabiki wao haiwezi kuelezeka.
Lakini kwa miaka mingi, filamu nyingi za Bollywood zimekuwa zikikosolewa kwa kuangazia mambo ya kizamani, yanayokuza chuki dhidi ya wanawake na upendeleo wa kijinsia.
Katika utafiti wake wa kwanza wa aina yake, watafiti kutoka Tiss (Taasisi ya Tata ya Sayansi ya Kijamii) huko Mumbai walijaribu kubainisha jinsi unyanyapaa wa mfumo dume ulivyokithiri kwenye sinema ya Kihindi.
Walichagua filamu 25 kati ya zile maarufu zaidi kutoka 2019, mwaka uliopita wa kabla ya janga, na filamu 10 zinazozingatia wanawake kati ya 2012 na 2019 - kipindi hicho kilichaguliwa ili kuona ikiwa kulikuwa na mabadiliko yoyote katika simulizi za filamu kufuatia genge la 2012- kubakwa kwa mwanafunzi wa kike kwenye basi huko Delhi, na ghasia zilizotokana na uhalifu huo na kuanzishwa kwa sheria mpya kali za kushughulikia uhalifu dhidi ya wanawake.
Orodha ya filamu ilijumuisha War, Kabir Singh, Mission Mangal, Dabangg3, Housefull4 na Ibara ya 15 na filamu zinazolenga wanawake ni pamoja na Raazi, Queen, Lipstick Under My Burkha na Margarita with a Straw, miongoni mwa zingine.
Watafiti walifuatilia karibu wahusika 2,000 kwenye skrini ili kuona nafasi zilizochezwa na waigizaji na kuchanganua filamu hizo kwa vigezo kadhaa kama vile dhana potofu ya ngono, ridhaa na ukaribu na unyanyasaji.
Walihesabu idadi ya filamu za LGBTQ+ na wahusika wake na jinsi walivyoonyeshwa, na kuchunguza ni wanawake wangapi walifanya kazi nyuma ya skrini kwenye filamu hizi.
Wamehitimisha kuwa ingawa filamu zinazowahusu wanawake zinatoa sababu fulani ya matumaini, filamu zilizotazamwa sana zinaendelea kuwa za udhalilishaji wa wanawake na za mawazo ya kizamani na uwakilishi wa wanawake na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja unasalia kuwa wa chini.
Kwa mfano, 72% ya wahusika katika filamu ambazo zilichanganuliwa ziliigizwa na wanaume, 26% wanawake na 2% ni waigizaji wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Watazamaji wengi wa filamu wanaaminika kuwa wanaume nchini India
Prof Lakshmi Lingam, kiongozi wa mradi wa utafiti huo, anasema "wanaopata pesa nyingi ni wanaume katika filamu za Bollywood" na watayarishaji wa filamu wanasema "mhusika wa kike mwenye nguvu sana hatashirikiana na watazamaji".
"Kuna hatua chache sana zinazochukuliwa kubadilisha hali kwa sababu kanuni za mfumo dume hubadilisha mawazo ya watu kuhusu hadithi au simulizi na wanaamini kwamba hii ndiyo inaweza kuwapa pesa," aliiambia BBC.
Kwa hivyo, anasema, wanashikamana na "mfumo" huo.
"Mhusika mkuu lazima awe mwanamume kutoka tabaka la juu, kiongozi wa kike awe mwembamba na mrembo. Anapaswa kuwa mcheshi na mwoga anayeonyesha ridhaa yake kwa ishara badala ya maneno, lakini anavaa mavazi yanayoonyesha umbo lake la kuvutia na lazima awe wa kisasa kumruhusu kuwa katika uhusiano wa kabla ya ndoa ambayo ni uvunjaji sheria."
Ajira kwenye filamu pia inafikiriwa kupitia mtazamo finyu wa kijinsia - Prof Lingam anasema ingawa "asilimia 42 ya viongozi wa kike waliajiriwa katika filamu hizi - [juu zaidi ya takwimu halisi za ajira za India za 25.1%] - walikuwa katika taaluma zenye dhana potofu".
"Wanaume tisa kati ya 10 walikuwa katika majukumu ya kufanya maamuzi wakichukua nafasi za maafisa wa jeshi, polisi, wanasiasa na wakuu wa uhalifu; wanawake wengi walikuwa madaktari na wauguzi, walimu na waandishi wa habari na ni mmoja tu kati ya 10 alikuwa katika majukumu ya kufanya maamuzi," anasema.
Taswira ya wahusika wa LGBTQ+, utafiti unaonyesha, bado imesalia kuwa tatizo kubwa - hawakuwa katika jukumu la kufanya maamuzi na mara nyingi walikuwa tu kwenye uoande wa ucheshi hasa masuala ya ngono.
Walemavu pia uwakilishi wao ulikuwa wa chini sana - walifikia 0.5% tu ya wahusika wote na wengi walitumiwa kama kuonyesha huruma au katika vichekesho.
"Watengenezaji filamu wanasema huo ndio ukweli. Lakini kuna ukweli mwingine mwingi ambao hawaonyeshi. Upo kati ya ukweli na kufirika ili kuhalalisha hali hii," Prof Lingam anasema.
Taswira ya wanawake na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja katika tasnia, anaongeza, lazima ibadilike kwa sababu "maisha halisi pia yanaamriwa na kile tunachokiona kwenye sinema".
"Nchini India, ambapo familia na shule hazifundishi juu ya elimu ya ngono na ridhaa, majibu yetu yote yanaathiriwa na vitabu na sinema," anasema, akiongeza kuwa ni shida wakati filamu kama Kabir Singh inamwonyesha kiongozi wa kiume akimvizia na kumnyanyasa shujaa ili kumtongoza.
"Inaonesha kuwa kawaida wanaume kuchukuliwa wenye nguvu. kwa hivyo mwanamke anaponyemelewa au kunyanyaswa mitaani, kila mtu anasema inatokea. Na huwa hakuna msukumo wowote."
Vidya Balan alihoji mfumo dume katika filamu yake Mission Mangal
Filamu chache ingawa, anadokeza, zinatoa taswira tofauti - kwa mfano, Mission Mangal, wakati mwanasayansi wa roketi, nafasi iliyochezwa na Vidya Balan, anazomewa na mkewe kwa kutumia muda mwingi kazini na kuwapuuza watoto wao na yeye na anageuka na kumuuliza ikiwa watoto sio jukumu lake pia.


Filamu za Queen na Lipstick Under my Burkha zilikuwa miongoni mwa filamu chache ambazo ziliongozwa na waigizaji wanawake na zilihusu wahusika wa kike wenye nguvu.
Lakini idadi ya filamu kama hizo bado ni ndogo sana.
Kwa upande mwingine, mfumo unaotumiwa na Bollywood haufanyi kazi tena.
"Filamu nyingi zinatawaliwa na wanaume zikiongozwa na baadhi ya waigizaji nyota wakubwa kama vile Salman Khan na Akshay Kumar zimefanya vizuri sana."
Kwa hivyo tasnia, anasema, inahitaji kufikiria tena maoni haya.
"Mawazo ya kawaida ni kwamba watazamaji wengi ni wanaume kwa hivyo filamu zinatengenezwa kwa ajili yao. Hatusemi usifanye filamu hizo, lakini fanya filamu nyingi ili kuwe na aina nyingi."
Sababu moja, anasema, kwa nini mwonekano wa Bollywood unajumuisha wanaume wengi, ni kwa sababu kuna wanawake wachache wanaofanya kazi nje ya skrini kwenye tasnia na wachache zaidi katika idara kuu za utengenezaji wa filamu - filamu ambazo Tiss ilifanya utafiti na kubaini zilikuwa na zaidi ya wanaume 26,300 na wanawake 4,100 pekee wafanyakazi.
"Ikiwa filamu zitatengenezwa kwa ajili ya hadhira tofauti, na watu mbalimbali nyuma ya skrini, simulizi pia zitakuwa tofauti," anasema Prof Lingam.

Wednesday 12 July 2023

Baraza la Sanaa Zanzibar: Wanaume Wanaosukwa kama Wanawake kukamatwa, faini ni Tsh. Milioni 1 au kifungo cha Miezi 6

 Member

1689135807959.png
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku tabia ya wanaume kusuka nywele na anayekamatwa faini yake ni Sh1 milioni au kifungu cha miezi sita au vyote kwa pamoja.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Julai 11, 2023, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Elimu na Utamaduni Zanzibar, Dk Omar Adam amesema hatua hiyo inalenga kulinda silika na tamaduni za Kizanzibari.

Amesema katazo hilo ni kwa mujibu wa sheria namba saba ya mwaka 2015 inayolenga kulinda utamaduni, mila na desturi za Mzanzibari bila kuathiri mambo mengine.

“Zanzibar hairuhusu mwanaume kusuka nywele faini ya kusuka nywele kwa Zanzibar ni Sh1 milioni au miezi sita jela au vyote kwa pamoja,” amesema.

Amesema hakuna kibali wala kulipia ili uruhusiwe kusuka nywele kwa mwanamme kama ambavyo awali ilisambaa kwennye mitandao ya kijamii.

“Sheria ilikuwa haijaanza kutekelezwa kwa kutoa faini lakini imeshatokea kama mara tatu mtu anakamatwa na kupewa onyo na wengine wapo wamejirekebisha na wengine wanaendelea kujirekebisha,” amesema

Hata hivyo, amesema katazo hilo haliwahusu Wamaasai kwasababu wanatambua kwamba huo ndio utamaduni wao kwamba mwanaume anasuka na mwanamke ananyoa au naye anasuka.

Kuhusu suala la kuathiri utalii wa Zanzibar, Katibu huyo amesema haliwezi kuathiri kwa sababu utafiti alioufanya kwanza watalii wengi hawasuki huo ni utamaduni ambao umetokea huku.

Kuhusu wasanii, amesema iwapo kuna msanii anataka kufanya shughuli zake wanaweza kukutana naye wakazungumza akavaa kofia mpaka anapokwenda kwenye maonyesho yake.

“Tunachosema suala la ushirikiano wa Muungano kisiwei kichaka cha kuharibu tamaduni silka na atamaduni za Kizanzibar ni akam ilivyo bangi hatuwezi kuruhusu kwamba ziendeel huku asili tuliochiwa na wazee wetu inapotea na katika sula hili tumejipanga tutakuwa wakali sana” alisema

Amesema watapitia hata kwenye shule kutoa elimu hiyo kwa walimu na wanafunzi ili kuwadhibiti wnafunzi wenye tabia hizo.

Sio mara ya kwanza kwa Zanzibar kutoa makatazo kama hayo, mwaka 2021 aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Musa alipiga marufuku kuvaa nguo fupi (nusu uchi) kwa watalii ili kulinda utamaduni wa Zanzibar

Agizo hilo lilitolewa, huku ikielezwa iwapo wakibainika wameevaa nguo zisizo na stara atakamatwa anayewatembeza na kutozwa faini, hata hivyo jambo hilo utekelzaji wake haukuzingatiwa.

Pia, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashidi Msaraka aliwahi kupiga marufuku vijana wanaonyoa viduku ambapo aliwahi kuwakamata na kuchukua mkasi kuwanyoa, hata hivyo nalo halikuwa na mwendelezo wake.

Tuesday 11 July 2023

Wanafunzi waliochelewa kuripoti shule ya wasichana ya Lucas Malia walala mtaani baada ya kuzuiwa kuingia

 

Nimekutana na ujumbe unasambaa kwenye mitandao ya kijamii Twitter, Instagram na hata JF nimeona mtu kaweka uzi kuwa wanafunzi tena wakike kutoka shule ya wasichana ya Lucas Malia walifungiwa mlango na hivyo kulazimika kulala nje sababu eti walichelewa kufika siku waliyotakiwa kuripoti shuleni. Tukio hilo limetokea Julai 9 na mpaka sasa hawajapolewa wako wanaranda tu mtaani.

download (2).jpg

Wakuu taarifa hii ni ya kweli?
Tunachokijua
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia ipo Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa Kata ya Mnacho. Shule ipo umbali wa kilometa 1 kutoka barabara kuu ya Ruangwa-Nanganga.

Ukifika kijiji cha Chimbila B. Shule ipo upande wa kulia ukitokea Nanganga na ipo kushoto ukitokea Ruangwa.

JUlai 11, 2023, Mtumiaji wa mtandao alitoa dokezo lililodai kuwa Shule ya Lucas Malia Lindi imekataa kupokea wanafunzi wa Kike walioripoti kwa kuchelewa. Hii ilikuwa ni Siku ya pili wanalala mitaani bila kujua hatma yao.

Kwenye dokezo hilo, baadhi ya wachangiaji walionesha kuunga mkono uamuzi wa shule hiyo wa kukataa kuwapokea wanafunzi hao walioripoti kwa kuchelewa huku baadhi wakilaani kitendo hicho kisicho cha kiungwana, ambacho ni hatari kufanyika kwa mtoto wa kike.

Undani wa tukio
Alipoulizwa  Mwalimu Mkuu, Gladness Makongwa, amesema;

“Siwezi kulizungumzia suala hilo kwenye simu, zaidi ya hapo naomba uzungumze na Mkurugenzi wa Halmashauri.”

Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Zuwena Omari Jiri, amesema;

“Taarifa iliwafikia wenzangu; Afisa Elimu wa Mkoa, Mkurugenzi na Afisa Elimu wa Wilaya, wameelekea Shuleni, watafanya kikao kujua kitu gani kimetokea na nini kinaendelea.”

Monday 10 July 2023

ATHUMANI AFUNGA NDOA NA WANAWAKE WA TATU SIKU MOJA

 ATHUMANI Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo.


Hali hiyo imeibua maswali na mshangao kwa wakazi wa Mpanda na jamii kwa ujumla ambapo baadhi ya watu wamesema tukio hilo nilakwanza kutokea kwa Katavi na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumzia ndoa yake Bwana harusi huyo amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na maumivu aliyoyapata mwanzo ya kuachwa na mke mmoja Aliekua amemuoa.

Amesema baada ya kuachwa na mke wake huyo aliona kuna umuhimu wa kuoa wanawake wanne ili ikitokea ameachwa na mmoja atabakia na wake watatu ndipo alipoanza kazi ya kuwatafuta wanawake hao kwa nyakati tofauti.

Senegal: Boti iliyobeba Wahamiaji 200 yapotea kwenye maji

 Waokoaji wa Uhispania wanaendelea na msako wa mashua hiyo karibu na Visiwa vya Canary ambapo inadaiwa haijulikani ilipo tangu ilipoanza safari zaidi ya wiki moja iliyopita.


Kundi la misaada la Walking Borders linasema boti hiyo ya wavuvi ilisafiri kutoka Mji wa Kafountine, Kusini mwa Senegal uliopo kilomita 1,700 kutoka Tenerife, ikidaiwa pia ilikuwa imebeba Kundi la Watoto kadhaa.


Wakati huohuo, boti nyingine mbili zilizobeba watu 65 na 60 nazo zinadaiwa kupoteza kwenye maji hivyo kufanya idadi ya watu ambao hawajulikani walipo ndani ya wiki moja

kuwa zaidi ya 325.

MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.

Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...