Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948

Saturday 15 July 2023

MARUFUKU KUFAA MAVAZI YANAYOFANANA NA YA KIJESHI


 Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limesema Katika siku za karibuni kumeibuka makundi ya watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya walinzi wa viongozi wakivaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama.


Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, kinakataza mtu yeyote ambaye si askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za majeshi ambapo ameongeza kuwa sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza pia.

Amesema Jeshi la Polisi Tanzania linawataka wale wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kinyume na sheria za nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitasita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Misime ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelee kuiweka nchi salama.

#2skys_updates 

No comments:

Post a Comment

MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.

Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...