Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948

Wednesday, 29 November 2023

Brookside Academy yaibuka Kinara

Shule ya Msingi Brookside iliyopo Kimara Suka, Wilaya ya Ubungo ,Jijini Dar es Salaam imedhamiria kuendelea kuwa mlipaji mzuri kwa kodi kwa lengo la kuchangia maendeleo ya taifa letu. Hivi karibuni shule hiyo ilikabidhiwa tuzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dar es Salaam ikiwa ni miongoni mwa mwa walipaji kodi bora hapa nchini. “Shule yetu imedhamiria kuendesha biashara zake kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa taifa,anasema Meneja wa Shule hiyo Masanja Maduhu. Meneja huyo anasema kuwa shule yake imedhamiria kuendelea kutoa elimu bora kwa wakazi wa Ki mara, Wilaya ya Ubungo na maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. “Natoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kuleta watoto wao kwenye shule yetu kwani tunawahakikishia elimu bora kwa vijana wao,” Shule hiyo inatoa elimu ya Awali na Msingi na kwamba wamedhamiria kuendelea kutoa elimu bora kwa wananchi. Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shule ya Awali na Msingi ya Brookside Masanja Maduhu akiwa amesimama na tuzo ya mlipaji kodi bora kwa mwaka huu, tuzo hizo zilikabidhiwa hivi karibuni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dar es salaam kwa walipaji kodi bora hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.

Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...