Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948

Tuesday 11 July 2023

Wanafunzi waliochelewa kuripoti shule ya wasichana ya Lucas Malia walala mtaani baada ya kuzuiwa kuingia

 

Nimekutana na ujumbe unasambaa kwenye mitandao ya kijamii Twitter, Instagram na hata JF nimeona mtu kaweka uzi kuwa wanafunzi tena wakike kutoka shule ya wasichana ya Lucas Malia walifungiwa mlango na hivyo kulazimika kulala nje sababu eti walichelewa kufika siku waliyotakiwa kuripoti shuleni. Tukio hilo limetokea Julai 9 na mpaka sasa hawajapolewa wako wanaranda tu mtaani.

download (2).jpg

Wakuu taarifa hii ni ya kweli?
Tunachokijua
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia ipo Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa Kata ya Mnacho. Shule ipo umbali wa kilometa 1 kutoka barabara kuu ya Ruangwa-Nanganga.

Ukifika kijiji cha Chimbila B. Shule ipo upande wa kulia ukitokea Nanganga na ipo kushoto ukitokea Ruangwa.

JUlai 11, 2023, Mtumiaji wa mtandao alitoa dokezo lililodai kuwa Shule ya Lucas Malia Lindi imekataa kupokea wanafunzi wa Kike walioripoti kwa kuchelewa. Hii ilikuwa ni Siku ya pili wanalala mitaani bila kujua hatma yao.

Kwenye dokezo hilo, baadhi ya wachangiaji walionesha kuunga mkono uamuzi wa shule hiyo wa kukataa kuwapokea wanafunzi hao walioripoti kwa kuchelewa huku baadhi wakilaani kitendo hicho kisicho cha kiungwana, ambacho ni hatari kufanyika kwa mtoto wa kike.

Undani wa tukio
Alipoulizwa  Mwalimu Mkuu, Gladness Makongwa, amesema;

“Siwezi kulizungumzia suala hilo kwenye simu, zaidi ya hapo naomba uzungumze na Mkurugenzi wa Halmashauri.”

Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Zuwena Omari Jiri, amesema;

“Taarifa iliwafikia wenzangu; Afisa Elimu wa Mkoa, Mkurugenzi na Afisa Elimu wa Wilaya, wameelekea Shuleni, watafanya kikao kujua kitu gani kimetokea na nini kinaendelea.”

No comments:

Post a Comment

MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.

Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...