ATHUMANI Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo.
Hali hiyo imeibua maswali na mshangao kwa wakazi wa Mpanda na jamii kwa ujumla ambapo baadhi ya watu wamesema tukio hilo nilakwanza kutokea kwa Katavi na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumzia ndoa yake Bwana harusi huyo amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na maumivu aliyoyapata mwanzo ya kuachwa na mke mmoja Aliekua amemuoa.
Amesema baada ya kuachwa na mke wake huyo aliona kuna umuhimu wa kuoa wanawake wanne ili ikitokea ameachwa na mmoja atabakia na wake watatu ndipo alipoanza kazi ya kuwatafuta wanawake hao kwa nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment