Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948

Wednesday 19 July 2023

TMA yatahadharisha uwepo wa El Nino kwa Asilimia 90, Oktoba 2023

TMA imesema hadi sasa imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hasa kipindi cha mvua za msimu wa vuli zinazotarajiwa kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu katika maeneo mbalimbali nchini. Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) imesema El Nino inatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu ambazo zitasababisha athari katika maeneo mbalimbali nchini. Akitoa taarifa hiyo leo Jumatano Julai 19, 2023 Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema hadi kufikia sasa inaonyesha imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Dk Kantamla aliyataja maeneo ambayo yataathirika na mvua za El nino ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara "Ongezeko la mvua linasababisha kutabiri uwepo wa El Nino, mfano kipindi cha kipupwe tumeona imeanza kujitengeneza athari zake hatutegemei kipindi hiki ongezeko la mvua kubwa,"amesema Dk Kantamla. Pia, Dk Kantamla amesema El Nino haitaathiri wakazi bahari ya hindi pekee itasambaa hadi maeneo ya nyanda za juu Kaskazini na ukanda wa Pwani. “Katika kipindi hiki cha kipupwe TMA inaendelea kufuatilia kwenye mchakato wa kuelekea msimu wa mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba mwaka huu na kuangaliwa athari za El Nino kwa ufasaha Ili kuifahamisha jamii kwa ujumla,”amesema. Nini maana ya El Nino Ni hali ya uwepo wa ongezeko la joto la bahari ya katika eneo la kati ya kitropiki la bahari ya Pasifiki, hali hii inapokuwepo kunakuwa na madhara mbalimbali katika maeneo tofauti ya duniani.

No comments:

Post a Comment

MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.

Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...