Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948

Sunday 8 October 2023

TAKRIBANI WATU 590 WAFARIKI KATIKA MAPIGANO YA ISRAEL NA HAMAS

ISRAEL/GAZA: ZAIDI YA WATadi hiyo inajumuisha vifo takriban 350 vya Raia wa Israel na Wapalestina zaidi 230 ambao wametajwa kupoteza maisha kufuatia majibizano ya Mashambulizi kati ya Kundi la HAMAS kutoka Palestina na Jeshi la Israel Mapigano yanaendelea hadi sasa ambapo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameapa kuzisambaratisha ngome zote za HAMAS zilizopo katika Mji wa Mpakani wa Gaza Ripoti zinaeleza kuwa zaidi ya Watu 2,000 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo. Hadi sasa HAMAS wanadai wanawashikilia zaidi ya Wapiganaji 100 wa Israel. ======= Gunmen from the Palestinian group Hamas rampaged through Israeli towns on Saturday, killing at least 250 Israelis and escaping with dozens of hostages in by far the deadliest day of violence in Israel since the Yom Kippur war 50 years ago. More than 230 Gazans were also killed when Israel responded with one of its most devastating days of retaliatory strikes. Fighting continued into the night. "We will take mighty vengeance for this wicked day," Prime Minister Benjamin Netanyahu said. Advertisement · Scroll to continue "Hamas launched a cruel and wicked war. We will win this war but the price is too heavy to bear," he said. "Hamas wants to murder us all. This is an enemy that murders mothers and children in their homes, in their beds. An enemy that abducts elderly, children, teenage girls." Hamas leader Ismail Haniyeh said the assault that had begun in Gaza, a narrow strip that is home to 2.3 million Palestinians, would spread to the West Bank and Jerusalem. Gazans have lived under an Israeli blockade for 16 years.

Tuesday 3 October 2023

Waziri Mwigulu: Ni marufuku kwa TRA kufunga Maduka

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema kitendo cha maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwafungia maduka wafanyabishara wadogo ni changamoto inayochochea kuwepo kwa uingizwaji holela wa bidhaa za magendo nchini. Nchemba amesema hayo jana Jumatatu Oktoba 2, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Njisi, Kasumulu katika mpaka wa Tanzania na Malawi, kwenye ziara aliyoambatana na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa. Hatua hiyo ya Nchemba imekuja kufuatia malalamiko ya wafanyabishara kufungiwa maduka kutokana na kushindwa kulipia leseni zao kwa wakati. “Naagiza TRA kuanzia sasa, acheni kuwasumbua wafanyabishara wadogo kwa kufunga maduka yao, kwani ni sehe,mu ya maisha yao, na pia wanasomesha watoto, sasa wekeni mifumo mazuri ya ukusanyaji wa kodi,” amesema na kuongeza; “Serikali imekuwa ikikusanya mapato kwa lengo la kusaidia kuboresha sekta binafsi, sasa endapo mkitumia mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kufunga maduka, hamtafikia malengo.” Nchemba amesema umefika wakati wa TRA kujenga uhusiano mazuri na wafanyabishara ikiwepo kutoa elimu au kuweka mfumo mzuri wa kulipia leseni hizo. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi amesema ujio wao katika Wilaya za Kyela na Rungwe, ni kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya miundombinu hususan barabara ya Ibanda mpaka Kajunjumele yenye urefu wa kilometa 22 inayonganisha bandari ya Kiwira na Itungi “Miradi hiyo itakapo kamilika itakuwa chachu ya kufungua fursa za kiuchumi hususan mwingiliano wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi,” amesema. Mfanyabiashara Ester Jordan, amesema kitendo cha Waziri wa Fedha kupiga marufuku TRA kuwafungia maduka, kutawafanya kulipa kwa wakati pindi wanapokuwa na uchumi mzuri. “Sio kwamba hatupendi kulipa kodi, hii ni nchi ambayo inajiendesha kwa kodi za watanzania, tunaomba tu uwekwe mfumo mzuri ili tusikinzane na Serikali,” amesema. Mawaziri hao wako mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kukagua miundombinu ya barabara katika Wilaya ya Rungwe na Kyela sambamba na mradi wa barabara njia nne kutoka Nsalaga Uyole mpaka Ifisi.

Sunday 1 October 2023

Moto mkubwa Kariakoo.

Habari za awali: Moto mkubwa ambao bado chanzo chake hakijajulikana, unaunguza maduka ya wafanyabiashara Kariakoo karibu na kituo cha mafuta cha Bigbon Msimbazi, jijini Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea jitihada kudhibiti moto huo, huku wafanyabiashara wakiendelea kuokoa baadhi ya bidhaa zao.

MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.

Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...