2SKYS INTERTAIMENT
Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948
2SKYS INTERTAIMENT
Kwa matangazo ya video na Picha .. 📱 Tupigie simu 0742100740 📧 Email Shafiishayani@gmail.com WhatsApp 0689079948
Thursday, 30 November 2023
MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.
Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi Magomeni ina madarasa mawili yaliyojengwa kwa nguzo za miti na kuezekwa kwa nyasi, madarasa hayo sasa yamebomolewa.
Oktoba 27, 2023, Mwandishi wa Habari hizi alifika katika shule hiyo na kukuta ina madarasa sita. Kati yake, mawili yamejengwa kwa hadhi hiyo ya nguzo za miti na nyasi.
Baada ya kushuhudia hali hiyo inayokinzana na miongozo ya kisera, ndipo Novemba 9, 2023, akautafuta uongozi wa wilaya hiyo kuchimbua undani wa kinachojiri shuleni Magomeni.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Chiza Marando, wote wakatoa ufafanuzi kwamba madarasa ya nyasi yaliyoshuhudiwa shuleni huko “ni mahali panapotumiwa na wanafunzi kula chakula”, lakini mwandishi alikuta kila darasa lina ubao wa kufundishia.
Hata hivyo, mwandishi aliporejea shuleni huko juzi (Novemba 19, 2023), alibaini madarasa hayo mawili ya nguzo za miti na paa la nyasi hayapo tena.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magomeni, Ibrahim Kinyonga (76), alipoulizwa kuhusu kilichotokea, alisema madarasa hayo yalibomelewa siku sita zilizopita na Kamati ya Shule kwa amri ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Magomeni.JPG
Magomeni3.JPG
Si rahisi kugundua kwamba kulikuwa na madarasa ya miti isipokuwa mashimo ya nguzo na ubao wa kuandikia uliojeng[1]wa kwenye ukuta wa darasa lililojengwa kwa matofali ya saruji na kuezekwa kwa bati.
Shule hii yenye wanafunzi 183 (wasichana 89), ina vyumba vinne vya madarasa yaliyojengwa kwa matofali ya saruji na kuezekwa kwa mabati, ambayo yameanza kuota kutu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Kinyonga, madarasa mawili ya miti na nyasi yaliyobomolewa yalijengwa miaka minne iliyopita na wananchi wa Kijiji cha Magomeni kwa mpango wa ku[1]jitolea ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Marando, alipoulizwa juzi sababu za kubomoa madarasa hayo alisema, “ni kweli niliagiza yabomolewe kwa kuwa si madarasa yanayohitajika shuleni. Yalijengwa kwa ajili ya mahali pa kulia chakula shuleni.”
Alisema madarasa hayo ya nguzo za miti na paa la nyasi, “yanatuletea image (sura) mbaya kwamba sisi Tunduru tuna madarasa ya nyasi. Kama kuna uhaba wa madarasa, hiyo ni issue (suala) nyingine.”
Mwandishi pia alibaini Shule ya Msingi Nambalapi ina ma[1]darasa yaliyoezekwa kwa nyasi. Mkurugenzi Marando alitoa ufafanuzi kuwa yamejengwa na wananchi kwa mpango wa dharura baada ya shule hiyo kukumbwa na mafuriko Mei mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magomeni (Kinyonga), anasema hajashirikishwa katika suala zima la kubomoa madarasa hayo na kwamba anashindwa kuelewa jinsi atakavyoeleza zoezi hili kwa wananchi.
Mago.JPG
Magomeni1.JPG
“Hapa ninashindwa kuelewa watoto wa darasa la awali hadi la VII watavyosoma katika vyumba vinne vilivyobaki. “Kwenye hayo madarasa ya nyasi walikuwa wanapishana, siku nyingine unakuta darasa la IV wanayatumia wakati mwingine la darasa la II, wengine wanakaa chini kwa sababu madawati ni machache,” anasema.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ezekiel Menge, alipotafutwa na mwandishi kuzungumzia hali ya miundombinu na samani shuleni, alisema walilazimika kutumia madarasa ya nyasi kufundisha wanafunzi kutokana na uhaba wa madarasa unaowakabili.
Katika vyumba vinne vya madarasa vilivyosalia, havitoshelezi wanafunzi 183 waliopo; sakafu imebomoka na mahali pengine pana mashimo: mada[1]wati ni machache na baadhi yamelegea kiasi kwamba mwa[1]nafunzi sharti ashikilie dawati lake wakati anaandika.
Plasta kwenye baadhi ya kuta imebanduka kiasi kwamba un[1]aweza kuhesabu idadi ya matofali. Katika moja ya madarasa ubao wa kuandikia unaning’nia kiasi cha kudondoka wakati wowote. Katika ofisi ya walimu ambako kuna meza mbili, kuna kiti kimoja tu (pichani) chenye ‘miguu mitatu’, mmoja umeshakatika.
Kinyonga anasema shule hii iliyosajiliwa mwaka 2002, ina walimu watano (wa kike wawili). Kati yao, watatu waaishi katika nyumba tatu zilizoko shuleni (moja ilijengwa na wanakijiji miaka mitano iliyopita).
Anabainisha kuwa mwalimu mmoja anaishi katika nyumba ya kupanga kijijini Magomeni na mwingine (wa kiume) anaishi Kijiji jirani cha Majimaji, takriban kilometa nane kutoka shuleni Magomeni.
Kuhusu huduma ya choo, Kinyonga anabainisha kuwa Shule ya Msingi Magomeni ina matundu sita ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi. Haina vyoo kwa ajili ya walimu wao. Wanatumia vyoo vilivyoko katika nyuma tatu za walimu.
Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, inaelekeza choo shuleni kitumike kwa uwiano wa 1:20, yaani tundu moja kwa wasichana 20 au 1:25 (tundu moja kwa wavulana 25).
Pia kila shule ina na vyoo kwa ajili ya walimu wa kike na wa kiume. Hivyo, kwa maelekezo hayo ya kisera, Shule ya Msingi Magomeni inapaswa kuwa na matundu manne kwa ajili ya wanafunzi wa kike 89 waliopo na manne mengine kwa ajili ya wanafunzi wa kiume 94 waliopo.
Pia inapaswa kuwa na choo kwa ajili ya walimu wao. Ibara ya 8(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inaelekeza wananchi kushiriki katika shughu[1]li za serikali yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hal[1]mashauri ya Wilaya ya Tunduru (Ma[1]rando), akizungumza hatua wanazo[1]chukua, alisema watajenga vyumba viwili vya madarasa katika shule hiyo mwaka huu wa fedha (2023/24) kwa kutumia mapato yao ya ndani.
Alisema wanahitaji Sh. bilioni 18 kukabili uhaba wa miundombinu na samani katika shule za msingi 153 za halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Marando alisema serikali inaendelea kuboresha miun[1]dombinu ya elimu wilayani Tunduru, ikiwapatia Sh. bilioni mbili mwaka 2022/23 na Sh. bilioni tatu mwaka huu wa fedha. Lakini hakuna fungu lililotengwa kwa ajili ya Shule ya Msingi Magomeni toka Serikali Kuu.
“Mwaka huu tutajenga madarasa mawili katika Shule ya Msingi Mago[1]meni kutokana na mauzo ya korosho. Mnada wa kwanza wa korosho tayari umefanyika, tumepata tani 15,000. Hapo tuna uhakika wa halmashauri kupata Sh. milioni 450 (wanatoza Sh. 30 kwa kila kilo ya korosho),” alisema Marando.
Alisema kipaumbele ni kwa shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi, akiitaja Shule ya Msingi Ligoma am[1]bako sasa wanatekeleza mradi wenye thamani ya Sh. milioni 513.2. Wana[1]jenga madarasa 14, matundu 24 ya vyoo, jengo la utawala na kichomea taka.
Pia wanajenga madarasa ya mawili ya mfano elimu ya awali na matundu sita ya vyoo. Mkurugenzi Marando pia alisema wanaendelea na ujenzi wa madarasa saba, matundu 14 ya vyoo, jengo la utawala na kichomea taka katika Shule ya Msingi Tinginya.
Mradi huo ambao pia unajumuisha ujenzi wa mtundu sita ya vyoo na madarasa mawili ya mfano elimu ya awali, unagharimu Sh. milioni 331.6.
Kimsingi, kinachoshuhudiwa shuleni Magomeni, si tu kinakinzana na maelekezo ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, bali pia ni ishara ya kutofanyiwa kazi hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2017.
Katika ripoti yake ya Ukaguzi Maalum wa Miundombinu na Samani za Shule za Msingi Tanzania aliyoitoa Machi 2017, CAG (kipindi hicho, Prof. Mussa Assad) alibainisha hali mbaya ya miundombinu na uhaba wa samani na walimu katika shule zinazomilikiwa na serikali. CAG alipendekeza serikali ichukue hatua za haraka kuboresha miundombinu iliyopo na kujenga mipya.
Wakati Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ikihitaji Sh. bilioni 18 kutatua changamoto ya uhaba wa miundombinu katika shule za msingi, uchambuzi wa Ripoti ya CAG kwa mwaka 2021/22 uliofanywa na Taasisi ya WAJIBU, umebaini Sh. bilioni 411.31 zimepotea katika mazingira yenye viashiria vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu katika matumizi ya kawaida, mishahara, mafao na rasili[1]mali watu nchini kwa mwaka huo wa fedha.
Kiasi hicho kilichopotea, kama kingeelekezwa kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni, kinatosha kujenga vyumba vya madarasa 20,565. Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, darasa moja linajengwa kwa Sh. milioni 20 likiwa na samani zake zote. Chanzo jamii forums
Wednesday, 29 November 2023
Brookside Academy yaibuka Kinara
Shule ya Msingi Brookside iliyopo Kimara Suka, Wilaya ya Ubungo ,Jijini Dar es Salaam imedhamiria kuendelea kuwa mlipaji mzuri kwa kodi kwa lengo la kuchangia maendeleo ya taifa letu.
Hivi karibuni shule hiyo ilikabidhiwa tuzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dar es Salaam ikiwa ni miongoni mwa mwa walipaji kodi bora hapa nchini.
“Shule yetu imedhamiria kuendesha biashara zake kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa taifa,anasema Meneja wa Shule hiyo Masanja Maduhu.
Meneja huyo anasema kuwa shule yake imedhamiria kuendelea kutoa elimu bora kwa wakazi wa Ki mara, Wilaya ya Ubungo na maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
“Natoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kuleta watoto wao kwenye shule yetu kwani tunawahakikishia elimu bora kwa vijana wao,” Shule hiyo inatoa elimu ya Awali na Msingi na kwamba wamedhamiria kuendelea kutoa elimu bora kwa wananchi.
Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shule ya Awali na Msingi ya Brookside Masanja Maduhu akiwa amesimama na tuzo ya mlipaji kodi bora kwa mwaka huu, tuzo hizo zilikabidhiwa hivi karibuni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dar es salaam kwa walipaji kodi bora hapa nchini.
Tuesday, 14 November 2023
Mvua kubwa Dar, kuanza kesho November 15.
Baada ya mapumziko ya siku mbili, mvua kubwa za El Nino sasa zinarejea tena Jijini Dar es Salaam na zitanyesha kwa siku nne mfululizo kuanzia kesho Novemba 15 na zitaendelea hadi Jumamosi ya Novemba 18 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA ni kwamba, mvua hizo mbali ya Dar es Salaam pia zitapiga katika mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Visiwa vya Unguja na Pemba ikijumuisha visiwa vya Mafia.
Mikoa mingine itakayokumbwa na mvua hizo kwa Jumatano ya Novemba 15 ni Njombe na Ruvuma ambapo athari zaidi ikiwemo mafuriko na baadhi ya shughuli za kiuchumi kusimama zitajitokeza siku ya Ijumaa.
TMA pia imetahadharisha mvua hizo kuweza kuambatana na upepo mkali unaofikia kasi ya Kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili ukanda wa Pwani ya Kusini ya Bahari ya Hindi mikoa ya Lindi na Mtwara.
Sunday, 8 October 2023
TAKRIBANI WATU 590 WAFARIKI KATIKA MAPIGANO YA ISRAEL NA HAMAS
ISRAEL/GAZA: ZAIDI YA WATadi hiyo inajumuisha vifo takriban 350 vya Raia wa Israel na Wapalestina zaidi 230 ambao wametajwa kupoteza maisha kufuatia majibizano ya Mashambulizi kati ya Kundi la HAMAS kutoka Palestina na Jeshi la Israel
Mapigano yanaendelea hadi sasa ambapo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameapa kuzisambaratisha ngome zote za HAMAS zilizopo katika Mji wa Mpakani wa Gaza
Ripoti zinaeleza kuwa zaidi ya Watu 2,000 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo. Hadi sasa HAMAS wanadai wanawashikilia zaidi ya Wapiganaji 100 wa Israel.
=======
Gunmen from the Palestinian group Hamas rampaged through Israeli towns on Saturday, killing at least 250 Israelis and escaping with dozens of hostages in by far the deadliest day of violence in Israel since the Yom Kippur war 50 years ago.
More than 230 Gazans were also killed when Israel responded with one of its most devastating days of retaliatory strikes. Fighting continued into the night.
"We will take mighty vengeance for this wicked day," Prime Minister Benjamin Netanyahu said.
Advertisement · Scroll to continue
"Hamas launched a cruel and wicked war. We will win this war but the price is too heavy to bear," he said. "Hamas wants to murder us all. This is an enemy that murders mothers and children in their homes, in their beds. An enemy that abducts elderly, children, teenage girls."
Hamas leader Ismail Haniyeh said the assault that had begun in Gaza, a narrow strip that is home to 2.3 million Palestinians, would spread to the West Bank and Jerusalem. Gazans have lived under an Israeli blockade for 16 years.
Tuesday, 3 October 2023
Waziri Mwigulu: Ni marufuku kwa TRA kufunga Maduka
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema kitendo cha maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwafungia maduka wafanyabishara wadogo ni changamoto inayochochea kuwepo kwa uingizwaji holela wa bidhaa za magendo nchini.
Nchemba amesema hayo jana Jumatatu Oktoba 2, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Njisi, Kasumulu katika mpaka wa Tanzania na Malawi, kwenye ziara aliyoambatana na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa.
Hatua hiyo ya Nchemba imekuja kufuatia malalamiko ya wafanyabishara kufungiwa maduka kutokana na kushindwa kulipia leseni zao kwa wakati.
“Naagiza TRA kuanzia sasa, acheni kuwasumbua wafanyabishara wadogo kwa kufunga maduka yao, kwani ni sehe,mu ya maisha yao, na pia wanasomesha watoto, sasa wekeni mifumo mazuri ya ukusanyaji wa kodi,” amesema na kuongeza;
“Serikali imekuwa ikikusanya mapato kwa lengo la kusaidia kuboresha sekta binafsi, sasa endapo mkitumia mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kufunga maduka, hamtafikia malengo.”
Nchemba amesema umefika wakati wa TRA kujenga uhusiano mazuri na wafanyabishara ikiwepo kutoa elimu au kuweka mfumo mzuri wa kulipia leseni hizo.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi amesema ujio wao katika Wilaya za Kyela na Rungwe, ni kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya miundombinu hususan barabara ya Ibanda mpaka Kajunjumele yenye urefu wa kilometa 22 inayonganisha bandari ya Kiwira na Itungi
“Miradi hiyo itakapo kamilika itakuwa chachu ya kufungua fursa za kiuchumi hususan mwingiliano wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi,” amesema.
Mfanyabiashara Ester Jordan, amesema kitendo cha Waziri wa Fedha kupiga marufuku TRA kuwafungia maduka, kutawafanya kulipa kwa wakati pindi wanapokuwa na uchumi mzuri.
“Sio kwamba hatupendi kulipa kodi, hii ni nchi ambayo inajiendesha kwa kodi za watanzania, tunaomba tu uwekwe mfumo mzuri ili tusikinzane na Serikali,” amesema.
Mawaziri hao wako mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kukagua miundombinu ya barabara katika Wilaya ya Rungwe na Kyela sambamba na mradi wa barabara njia nne kutoka Nsalaga Uyole mpaka Ifisi.
Sunday, 1 October 2023
Moto mkubwa Kariakoo.
Habari za awali: Moto mkubwa ambao bado chanzo chake hakijajulikana, unaunguza maduka ya wafanyabiashara Kariakoo karibu na kituo cha mafuta cha Bigbon Msimbazi, jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea jitihada kudhibiti moto huo, huku wafanyabiashara wakiendelea kuokoa baadhi ya bidhaa zao.
Wednesday, 23 August 2023
Mbeya Achomwa moto , kwa kubaka
Kijana mmoja ambaye jina lake halijajulikana, ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akimlawiti mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano na kumsababishia kifo.
Tukio hilo limetokea Isanga jijini Mbeya na kuzua taharuki kubwa, ikielezwa kwamba kumekuwa na mfululizo wa matukio ya watoto kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika mtaa huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI MAGOMENI.
Wiki mbili baada ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe kuzungumza na uongozi wa Wilaya ya Tunduru kutaka kujua kwanini Shule ya Msingi...
-
TMA imesema hadi sasa imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hasa kipindi cha mvua za msimu wa vuli zinazotarajiwa kunyesha Oktoba hadi ...
-
Habari za awali: Moto mkubwa ambao bado chanzo chake hakijajulikana, unaunguza maduka ya wafanyabiashara Kariakoo karibu na kituo cha mafuta...
-
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema kitendo cha maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwafungia maduka wafanyabishara wadogo ni changamo...